MCHORO 19.2: CHAGUO ZA NAFUU KWA MPIRA USIOWEZA KUCHEZWA KATIKA ENEO LA KAWAIDA
Mchezaji anaamua kuwa mpira wake ulioko ndani ya kichaka hauwezi kuchezwa. Mchezaji ana chaguo tatu, ambapo katika kila chaguo ataongezewa mpigo mmoja wa adhabu. Mchezaji anaweza:
- Kuchukua nafuu ya mpigo-na-umbali kwa kucheza mpira kutoka eneo la nafuu linalotegemea mahali mpigo wa awali ulipochezwa.
- Kuchukua nafuu ya kurudi-nyuma-kwenye-mstari kwa kudondosha mpira nyuma ya mahali ulipokuwa mpira wa awali, huku ukihakikisha kuwa mahali ulipokuwa mpira wa awali panabaki kati ya shimo na sehemu ambayo mpira unadondoshwa.
- Chukua nafuu ya pembeni. Sehemu ya marejeleo ya kuchukua nafuu ni mahali ulipokuwa mpira wa awali, na mpira lazima udondoshwe na kuchezwa kutoka eneo la nafuu la urefu wa fimbo mbili, ambalo haliko karibu zaidi na shimo kuliko sehemu ya marejeleo.