Lengo la Kanuni:Kanuni ya 1 inatambulisha misingi kuu ya mchezo kwa mchezaji:
Cheza uwanja kama unavyoukuta na ucheze mpira kama ulivyolala.
Cheza kwa kufuata Kanuni na kwa kuzingatia roho ya mchezo.
Wewe ndiye unawajibika kujiongezea adhabu unapokiuka Kanuni, ili usipate faida yoyote dhidi ya mpinzani wako katika mechi ya match play au dhidi ya wachezaji wengine katika stroke play.