Unapochukua nafuu ya kutochezeka katika banka, ni chaguo gani kati ya zifuatazo litakuwa na jumla ya adhabu ya mapigo mawili?
A
Nafuu ya pembeni ndani ya banka.
B
Nafuu ya mstari wa nyuma nje ya banka.
C
Nafuu ya mpigo-na-umbali nje ya banka.
2/10
Ni ipi kati ya zifuatazo iliyo sahihi?
A
Nafuu bila adhabu hauwezi kuchukuliwa kutoka kwa maji ya muda ndani ya banka.
B
Mchezaji anaweza kudondosha mpira nje ya banka bila adhabu anapochukua nafuu kutoka kwa maji ya muda ndani ya banka.
C
Mchezaji anaweza kudondosha mpira nje ya banka, akiongeza mkwaju mmoja wa adhabu, anapochukua nafuu kutoka kwa maji ya muda ndani ya banka.
3/10
Ni ipi kati ya zifuatazo iliyo sahihi?
A
Kizuizi kinachoweza kusogezwa kinaweza kuondolewa kutoka ndani au nje ya uwanja.
B
Kizuizi kinachoweza kusogezwa kinaweza kuondolewa tu kikiwa uwanjani.
C
Kizuizi kinachoweza kusogezwa kinaweza kuondolewa tu kutoka kwenye grini.
4/10
Ni ipi kati ya zifuatazo si kikwazo kinachoweza kuondolewa?
A
Mfuko wa plastiki.
B
Ganda la ndizi.
C
Reki.
5/10
Unapochukua nafuu ya adhabu kutoka kwenye eneo la adhabu jekundu, ni chaguo gani linalokuruhusu kuachilia mpira katika eneo la nafuu lenye urefu wa fimbo mbili,wakati mpigo wa awali ulifanyika kutoka kwenye uwanja wa kati?
A
Nafuu ya mpigo-na-umbali.
B
Nafuu ya mstari wa nyuma.
C
Nafuu ya pembeni.
6/10
Unapochukua nafuu ya mpigo-na-umbali, lipi kati ya yafuatayo si la kweli?
A
Unapocheza tena kutoka eneo la kuanzishia mpira lazima uchezwe kutoka mahali popote ndani ya eneo la kuanzishia mpira (teeing area).
B
Unapocheza tena kutoka eneo la jumla, mpira lazima udondoshwe karibu iwezekanavyo na mahali ambapo mpigo wa mwisho ulifanywa.
C
Unapocheza tena kutoka kwenye grini, mpira lazima uwekwe mahali palepale ambapo mpigo wa awali ulifanywa.
7/10
Katika match play, wewe na mpinzani wako mnakubaliana jinsi ya kuamua suala la kanuni linalohusiana na mpira wako, ijapokuwa hakuna kati yenu anayejua kwa hakika kanuni sahihi. Baada ya kushinda mechi, unagundua kuwa mlitafsiri vibaya kanuni hiyo, uamuzi ni upi?
A
Matokeo ya mechi yanasalia kama yalivyochezwa.
B
Lazima usahihishe uamuzi na hali ya mechi. Ikiwa ni lazima, ni sharti urudi uwanjani ili kuendeleza mechi.
C
Unapoteza mechi.
8/10
Anapochukua nafuu kwa mpira uliopenyea ardhini, mchezaji anaweza kudondosha mpira hadi urefu wa fimbo moja kutoka sehemu iliyo moja kwa moja nyuma ya mahali mpira ulipokuwa?
A
Kweli.
B
Si kweli.
9/10
Unapochukua nafuu kutoka eneo chini ya ukarabati katika eneo la jumla, ni ipi kati ya kauli zifuatazo si ya kweli?
A
Lazima udondoshe ndani ya urefu wa fimbo mbili kutoka sehemu ya karibu kabisa ya nafuu kamili.
B
Lazima udondoshe mpira katika eneo la jumla.
C
Unaweza chagua kudondosha mpira wa awali au mpira mwingine.
10/10
Huruhusiwi kucheza mpira wa akiba katika hali gani?
A
Wakati mpira wako unaweza kuwa umepotea katika eneo la jumla.
B
Wakati mpira wako unaweza kuwa nje ya mipaka.
C
Wakati mpira wako unajulikana kuwa katika eneo la adhabu.